Kikosi cha Twiga Stars
Timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twigs Stars) inatarajia kuondoka Agosti 31 mwaka huu kwenda Maputo, Msumbiji kwenye michezo ya All Africa Games itakayofanyika nchini humo kuanzia Septemba 3-18 mwaka huu.
Twiga Stars katika msafara wake itakuwa na jumla ya watu 20 ambapo kati yao 16 ni wachezaji na wanne ni viongozi wakiwemo Kocha Mkuu Charles Boniface na msaidizi wake Nasra Mohamed.
Mechi ya kwanza ya Twiga Stars itakuwa Septembe 5 mwaka huu dhidi ya Ghana wakati ya pili dhidi ya Afrika Kusini itachezwa Septemba 8 mwaka huu. Twiga Stars itacheza mechi yake ya mwisho katika hatua ya makundi Septemba 11 mwaka huu dhidi ya Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment