Saturday, August 27, 2011

CHEKA AMTANDIKA WANYONYI

Bondia Francis Cheka (mwenye glov nyekundu) akirusha 'kombora' kwa Daniel Wanyoni kutoka Kenya, katika pambano lililopigwa jana usiku.


BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Francis Cheka SMG juzi usiku aliendeleza rekodi yake ya ushindi baada ya kumshinda Mkenya, Daniel Wanyonyi kwa pointi kwenye pambano lililokuwa sio la ubingwa.

Pambano hilo lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na kushuhudiwa na maelfu ya mashabiki na wapenzi wa ngumi walishangilia dakika zote za mchezo huo wa raundi kumi uliotawaliwa zaidi na Cheka.

Cheka alishinda pambano hilo kwa pointi baada ya majaji wote watatu wa mchezo huo kumpa Cheka pointi 100, huku majaji hao wakitofautiana katika pointi za Wanyonyi, ambapo Ibrahim Kamwe alimpa alama 95, Omari Yazidu alimpa pointi 93 na Kondo Nassoro alimpa pointi 93.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa pambano hilo Cheka alisema siku zote hujiandaa kushinda na sio vinginevyo nia yake ni kuwapa raha mashabiki wake wa ngumi kwani anapokuwa ulingoni huwa makini na kazi anayoifanya.

ìTangu awali nilimtahadharisha Wanyonyi kuwa mimi ni moto wa kuotea mbali akabisha, lakini baada ya kipigo hiki nadhani sasa atakubali kauli yangu,îalisema bondia Cheka huku akicheka.
Mpaka sasa Cheka ameshacheza mapambano 31, ambapo kati ya hayo 15 ameshinda kwa KO, mapambano nane alishinda kwa pointi, huku sita akiwa amepoteza na mawili akiwa ametoa sare.

Pia, Cheka anashikilia mikanda ya ICB, WBO pamoja na UBO na na anatarajiwa kuendelea na mazoezi yake kwa ajili ya kujiandaa na pambano dhidi Bondia Mada Maugo pambano linalotarajiwa kufanyika mapema Septemba mwaka huu mjini Morogoro.

No comments:

Post a Comment