HAPA NI BAADA YA KUFANYIWA UTAMBULISHO
WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO WAKIKUSANYA USHAHIDI KWA AJILI YA KUIFAHAMISHA DUNIA.......HATIMAYE CSEC FABREGAS AMEJIUNGA NA BARCELONA BAADA YA KUHUSISHWA NA KURUDI KWA TIMU YAKE YA ZAMANI KWA TAKRIBANI MISIMU MITANO ILIYOPITA, NA LEO AMETAMBULISHWA RASMI KWA WAANDISHI WA HABARI NA MASHABIKI WA TIMU KWENYE UWANJA NOU CAMP-CATALAN SPAIN. WAKATI HUO HUO
Masaa machache tangu ajiunge rasmi na Barcelona, Cesc Fabregas amewaomba radhi mashabiki wa klabu ya Arsenal kwa kutowaambia lolote juu ya uhamisho wake kwenda Barcelona huku akiahaidi kuwapa sababu zilizomfanya ahame kwenye klabu ndani ya siku chache zijazo.
Fabregas ambaye alikuwa nahodha wa Arsenal amerudi Barca baada ya kuwepo Emirate kwa takribani miaka 8 na hatimaye jana Jumatatu alimaliza utata wa uhamisho wake kwenda Catalunya.
Kiungo huyo Spain anasema uongozi wa Arsenal waliweka sheria kali juu ya kuongelea uhamisho wake na ndio maana alishindwa kuzungumza chochote.
Fabregas anakiri ulikuwa ni uamuzi mgumu kuondoka Emirates Stadium na anasema atawaambia mashabiki wa Gunners ukweli wote kuhusu uhamisho wake wa kujiunga na Barca.
“Nina muda wa kuzungumza juu ya suala hili na uhakika nitafanya interview maalum kwa ajili ya kuwaambia story yote mashabiki wa Arsenal kuhusu uhamisho wangu.
“Samahani sikuweza kusema chochote katika kipindi chote cha miezi miwili na nusu, Arsenal walinikataza kuzungumza lolote kuhusu uhamisho wangu hata kama nilikuwa nataka kufanya hivyo lakini nilishindwa.
No comments:
Post a Comment