Wednesday, August 31, 2011

MRUSI ASHINDA MASHINDANO YA 'KUPIGA KWATO'

Daegu

Katika siku ya tano mashindano ya Ubingwa wa riadha wa dunia haya kulikuwa na mashindano ya mbio za fainali za kutembea za kilomita 20 kwa wanawake. Ushindi umemwendea Mrusi Olga Kaniskina baada ya kwenda kasi ya saa moja dakika 29 na sekunde 42.
Baada ya mashindano alisema kuwa mpambano ulikuwa mkali kwake akilinganisha na mashindano ya Osaka na Berlin.Amesema kuwa kulikuwa na jua kali na hata hivyo amehimili na kushinda sasa anataka kuwa ubingwa wa Ulaya.
Nafasi ya pili ilikwenda kwa Mchina Hong LIU ambae katika mashindano ya Berlin, miaka miwili iliopita, alishika nafasi ya tatu.
Nafasi ya tatu ilikwenda Urusi .
Susana Feitur kutoka Ureno hajaishiwa nguvu licha ya kushiriki mara 11 mfululizo na bila kushinda . Amemaliza wa sita, na anaona kidogo anapiga hatua mbele kwani katika mashindano ya Berlin 2009 alikuwa wa 10.
Mkenya pekee katika mashindano haya ambayo kawaida si ya Afrika ni Grace wanjiru Njue ambae hakufua dafu karibu alikuwa wa mwisho.

No comments:

Post a Comment