Kikosi cha Twiga Stars
Timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twigs Stars) inayoondoka Agosti 31 mwaka huu kwenda Maputo, Msumbiji kwenye michezo ya All Africa Games itakayofanyika nchini humo kuanzia Septemba 3-18 mwaka huu itaagwa kesho (Agosti 30 mwaka huu).
Twiga Stars wataagwa saa 6 mchana kambini kwao hoteli ya Itumbi iliyopo Magomeni Mwembechai, Dar es Salaam. Wakati huo huo Kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza majina ya wachezaji 16 watakaokwenda Maputo.
Wachezaji hao ni Sophia Mwasikili, Fatuma Omary, Mwanaidi Tamba, Fatuma Bashiri, Mwajuma Abdallah, Asha Rashid, Mwanahamisi Omari, Pulkeria Charaji, Ester Chabruma, Zena Khamis, Fridian John, Fatuma Mustafa, Ettoe Mlenzi, Ftuma Khatib, Maimuna Said na Mwapewa Mtumwa.
Viongozi watakaofuatana na timu hiyo ni Mkwasa, kocha msaidizi Nasra Mohamed, daktari wa timu Dk. Gania Seif wakati Meneja wa timu hiyo ni Furaha Francis.
Mechi ya kwanza ya Twiga Stars itakuwa Septembe 5 mwaka huu dhidi ya Ghana wakati ya pili dhidi ya Afrika Kusini itachezwa Septemba 8 mwaka huu. Twiga Stars itacheza mechi yake ya mwisho katika hatua ya makundi Septemba 11 mwaka huu dhidi ya Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment