Aifungia Chelsea bao katika mechi yake ya kwanza Stamford Bridge
Juan Mata katika mechi yake ya kwanza katika uwanja wa Chelsea wa Stamford Bridge, aliweza kufunga bao lake la kwanza akiichezea timu yake mpya, na kuiwezesha kusonga hadi kuongoza ligi kuu ya Premier, baada ya kuifunga Norwich magoli 3-1.
Hata hivyo, licha ya kupata ushindi, mashabiki wengi wanafikiria kwamba Chelsea haikucheza kama ilivyotazamiwa.Chelsea walikuwa wa kwanza kupata bao, kupitia mchezaji Jose Bosingwa, lakini Norwich wakasawazisha kupitia mchezaji Grant Holt.
Frank Lampard alitia wavuni mkwaju wa penalti na kuongeza mabao hadi 2-1, baada ya kipa John Ruddy kumwangusha Ramires, akihisi mchezaji huyo wa Chelsea alikuwa anajiandaa kufunga.
Mata aliiandikishia Chelsea ushindi, lakini raha ya ushindi huo kugubikwa na kutojua hali ya Didier Drogba ni vipi, baada ya kujeruhiwa kichwa.
Kipa Ruddy alikuwa anajaribu kuondosha mpira alipompiga ngumi ya uso Drogba.
Katika mechi nyingine, Aston Villa na Wolves walishindwa kufungana, na mechi kwisha 0-0.
Matokeo yalikuwa ni kama hayo pia katika mechi kati ya Swansea na Sunderland.
Everton iliwafunga Blackburn goli 1-0.
Wigan nayo iliwafunga QPR magoli 2-0.
Pambano la mwisho katika ratiba ya Jumamosi lilikuwa ni kati ya Liverpool na Bolton ambapo Liverpool walichomoza na ushindi wa mabao 3 - 1, mabao ya Liverpool yakifungwa na Jordan Henderson dk15, Martin Skrtel dk52 na Charlie Adam dk53 wakati bao la kufutia machozi kwa upande wa Bolton likifungwa na Ivan Klasnic dk90. Msimamo ulivyo mpaka sasa baada ya michezo ya jana ni kama ifuatavyo;
Msimamo wa Ligi Kuu ya England
Position | Timu | M | TG | PNT |
---|---|---|---|---|
1 | Liverpool | 3 | 4 | 7 |
2 | Chelsea | 3 | 3 | 7 |
3 | Wolves | 3 | 3 | 7 |
4 | Man City | 2 | 5 | 6 |
5 | Man Utd | 2 | 4 | 6 |
6 | Aston Villa | 3 | 2 | 5 |
7 | Wigan | 3 | 2 | 5 |
8 | Newcastle | 2 | 1 | 4 |
9 | Bolton | 3 | 1 | 3 |
10 | Everton | 2 | 0 | 3 |
11 | QPR | 3 | -5 | 3 |
12 | Stoke | 2 | 0 | 2 |
13 | Sunderland | 3 | -1 | 2 |
14 | Norwich | 3 | -2 | 2 |
15 | Swansea | 3 | -4 | 2 |
16 | Arsenal | 2 | -2 | 1 |
17 | Fulham | 2 | -2 | 1 |
18 | West Brom | 2 | -2 | 0 |
19 | Tottenham | 1 | -3 | 0 |
20 | Blackburn | 3 | -4 | 0 |
No comments:
Post a Comment