Thursday, August 25, 2011

FERGUSON AKUBALI YAISHE KWA BBC

Sir Alex Ferguson - Kocha wa Manchester United
Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson amekubali kuanza kuzungumza na BBC.
Ferguson alianza kususia kuzungumza na BBC mwaka 2004 baada ya kituo hicho kutoa tuhuma dhidi ya mwanae, Jason, katika kipindi kimoja cha televisheni.
Taarifa iliyotolewa imesema: "Sir Alex na BBC wameweka kando tofauti zao ambazo zilisababisha Sir Alex kutojisikia kuzungumza na BBC na vipindi vyake."
Manchester United inacheza na Arsenal siku ya Jumapili kwenye uwanja wa Old Trafford.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa siku ya Alhamisi, inafuatia mazungumzo kati ya Sir Alex na mkurugenzi mkuu wa BBC, Mark Thompson, na mkurugenzi wa BBC kanda ya kaskazini Peter Salmon.
Taarifa hiyo imeongeza: "Suala hilo limefikia muafaka na pande zote mbili kuridhia.
"Sir Alex sasa atakuwa akiweza kuzungumza katika kipindi cha BBC Match of The Day, Radio 5 live na vyombo vingine vya BBC kama ilivyokubaliwa.
"Hakuna maelezo zaidi yatatolewa na pande mbili hizo kuhusiana na suala hilo." imemaliza taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment