Monday, August 29, 2011

ARSENAL YAKUTANA NA MAAFA MAZITO KUTOKA KWA MAN UTD, YASHINDILIWA 'MISUMARI' 8-2!

Ashley Young na Wayne Rooney

Wayne Rooney amepachika mabao matatu peke yake wakati Manchester United ikiinyuka Arsenal kwa mabao 8-2.
Danny Welbeck ndiye alifungua karamu ya magoli baada ya kuunganisha pasi ya Anderson.
David De Gea aliokoa penati iliyopigwa na Robin Van Persi, na baadaye kidogo Ashely Young kufunga bao la pili.
Rooney aliandika bao la tatu na la nne kwa mikwaju miwili ya adhabu, kabla ya kufunga bao moja kwa mkwaju wa penati.
Nani na Park Ji Sung walifunga nao na Ashley Young kuongeza jingine.
Mabao ya Arsenal yalifungwa na Theo Walcott na Robin Van Persie.
Wachezaji wa Man City wakeshangilia ushindi


Awali Manchester City waliizaba Tottenham Hotspur kwa mabao 5-1.
Edin Dzeko alifunga mabao manne, na Sergio Aguero akifunga moja. Bao pekee la Spurs lilifungwa na Younis Kaboul.
Wachezaji wa Newcastle United

Kwingineko Newcastle United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fulham. Leon Best akifunga mabao yote ya Newcastle na goli la Fulham kufungwa na Clint Dempsey.
West Brom walishindwa kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kuchapwa bao 1-0 na Stoke City. Goli hilo pekee lilifungwa na beki Ryan Shotton katika dakika ya 89. Msimamo ulivyo baada ya matokeo ya jana ni kama unavyoonekana hapo chini;

Msimamo wa Ligi Kuu ya England

Jumatatu, 29 Agosti.
PositionTimuMTGPNT
Full Msimamo wa Ligi Kuu ya England
1Man Utd3109
2Man City399
3Liverpool347
4Chelsea337
5Wolves337
6Newcastle327
7Aston Villa325
8Wigan325
9Stoke315
10Bolton313
11Everton203
12QPR3-53
13Sunderland3-12
14Norwich3-22
15Swansea3-42
16Fulham3-31
17Arsenal3-81
18West Brom3-30
19Blackburn3-40
20Tottenham2-70

No comments:

Post a Comment