Friday, August 26, 2011

ALGERIA KUWASILI SEPTEMBA MOSI NCHINI

Timu ya Taifa ya Algeria walipokutana na England katika fainali za Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini 2010

Algeria ‘Desert Warriors’ inatarajia kuwasili nchini Septemba Mosi mwaka huu saa 1 jioni kwa ndege ya kukodi ikiwa na msafara wa watu 50 ambapo kati yao 25 ni wachezaji. Timu hiyo itafikia kwenye hoteli ya Golden Tulip.
 
Mechi kati ya Taifa Stars na Algeria itachezwa Septemba 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili. Pambano hilo ni la mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon. Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Algiers timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
 
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Nicholas Musonye kutoka Kenya wakati waamuzi ambao wote wanatoka Mauritania ni Ali Lemghaifry, Mohamed Hamada, Hassane el Dian a Pene Cheikh Mamadou.

No comments:

Post a Comment