Wednesday, August 31, 2011

DIRISHA LA USAJILI LAFUNGWA: CHELSEA WANASA SAINI YA MEIRELES DAKIKA YA MWISHO, WRIGHT-PHILLIPS ATUA QPR, LIVERPOOL YAMKAMATA CRAIG BELLAMY WA MAN CITY, YOSSI BENAYOUN WA CHELSEA AMWAGA WINO ARSENAL......

 Chelsea Football Club is delighted to announce the signing of Raul Meireles from Liverpool on a four-year contract.
 Shaun Wright-phillips has completed a move to Queens Park Rangers from Manchester City and admits he cannot wait to get started.
Arsenal have completed the signing of Israeli international Yossi Benayoun with the Chelsea. 
 Carlos Tevez - Not leaving Man City

Wesley Sneijder - Not leaving Inter Milan.

Arsenal have agreed an £8million transfer fee for defender Per Mertesacker with Werder Bremen.


Liverpool have confirmed the signing of former player Craig Bellamy as the Man City man agrees a contract and completes his much anticipated move to Merseyside.



Luka Modric - Not leaving Tottenham

The England midfielder joins as a free agent having left Manchester United at the end of last season. He has put pen to paper on a one-year contract and will train on Thursday.
Sky Sports sources understand that Peter Crouch has agreed to join Stoke and is waiting to finalise a switch from Tottenham.
 Mikel Arteta - Left
SOMA ZAIDA KUHUSU USAJILI
Goal.com's Top 20 Transfers of Summer 2011

SIKU YA MWISHO YA USAJILI ENGLAND, FUATILIA NANI KAENDA WAPI NANI KABAKI WAPI

Mauro Zarate 
Asamoa Gyan
 Nicklas Bendtner
Scott Dann 
Diego 
Peter Crouch
Per Mertesacker
Manuel Giandonato
 Franck Ribery
 Joe Cole
 Reto Ziegler
Pedro Leon.
Simon Kjaer   



BARCELONA YAANZA NA MAUAJI LA LIGA, YAIKANDAMIZA VILLARREAL 5-0!

Wachezaji wa FC Barcelona wakishangilia kumpongeza Lionel Messi wa Argentina kufunga bao katika mechi yao ya ufunguzi ya Ligi Kuu Hispania, La Liga dhidi ya Villarreal kwenye Uwanja wa Camp Nou mjini Barcelona, Hispania jana Jumatatu. Barca ilishinda 5-0.
Barcelona waliifunga Villareal bila hururma kwa mabao 5-0 na kuwajibu wapinzani wao Madrid ambao waliwafunga Zaragoza mabao 6-0.
Pep Guardiola aliwakosa Dani Alves , Carles Puyol na Gerard Pique hivyo akamchezesha Eric Abidal na akawatumia Sergio Busquets na Javier Mascherano kwenye ulinzi.
Xavi Hernandez na David Villa waliwekwa benchi huku Thiago Alcantara, Cesc Fabregas na Alexis Sanchez wote wakianza .
Juan Carlos Garido alipanga timu ile ile ya Villareal iliyotegemewa na wengi ambapo Bruno Soriano alirudi kwenye sehemu yake ya kiungo baada ya kuwa amecheza kaka beki katikati ya wiki na Gonzalo Rodriguez alirudi kucheza beki.

Mchezo huu ulikuwa si wa ushindani kama ule uliozikutanisha timu hizi mwaka jana . Villareal walikuwa hawana mashambulizi kabisa na walifia mikononi mwa Barca kwa urahisi ambao hakuna aliyeutegemea. Wafungaji wa mabao hayo ni:
 
 
 
 

11 WATEULIWA KUTATHMINI WAAMUZI LIGI KUU

Kamati ya Waamuzi ya TFF imeteua watathmini 11 wa waamuzi (referees assessors) kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom. Watathmini hao watasimamia baadhi ya mechi za ligi hiyo.
Waamuzi wa ligi Kuu ya Vodacom wakitoka uwanjani chini ya ulinzi mkali wa Polisi
Walioteuliwa ni Alfred Lwiza (Mwanza), Soud Abdi (Arusha), Charles Mchau (Kilimanjaro), Manyama Bwire (Dar es Salaam), Joseph Mapunda (Ruvuma), Isabela Kapela (Dar es Salaam), Paschal Chiganga (Mara), Emmanuel Chaula (Rukwa), Mchungaji Army Sentimea (Dar es Salaam), David Nyandwi (Rukwa) na Leslie Liunda (Dar es Salaam).

IVAN KNEZEVIC WA FK BORAC AOMBEWA ITC

Aliyekuwa kipa wa Yanga, Ivan Knezevic
Aliyekuwa kipa wa Yanga, Ivan Knezevic ameombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) na Chama cha Mpira wa Miguu cha Serbia (FAS) ili kujiunga na klabu yake mpya nchini humo.
 
Knezevic ameombewa ITC kama mchezaji wa ridhaa katika klabu ya FK Borac ya nchini humo. TFF itampatia hati hiyo kwa vile mkataba wake katika klabu ya Yanga ulikuwa umemalizika.
 

HUKUMU YA RAGE NA SENDEU YAPIGWA KALENDA!

Ismail Aden Rage - Mwenyekiti wa Klabu ya Simba
Afisa habari wa klabu ya Yanga, Luis Sendeu (kushoto), Mwenyekiti wa Yanga Nchunga (katikati )na Makamu Mwenyekiti Mosha wakiwa klabuni Yanga
Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti wake Alfred Tibaigana iliyokuwa ikutane jana kusikiliza malalamiko dhidi ya Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage na Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu imeahirisha kikao chake.
 
Kwa mujibu wa Tibaigana, kikao kimeahirishwa kutokana na Kamati kutotimiza akidi (column) kwa wajumbe wake. Walalamikiwa wataarifiwa siku ambayo kikao kitapangwa tena.


ALGERIA KUWASILI DAR USIKU!

Algeria wakipambana na England 2010

Timu ya Taifa ya Algeria (Desert Warriors) itawasili Septemba Mosi mwaka huu saa 2.50 usiku kwa ndege maalum. Algeria itacheza mechi ya mchujo kuwania tiketi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon.
Kikosi cha Algeria kitakachovaana na Stars Septemba 3

Mechi hiyo itachezwa Septemba 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Viingilio kwa mechi hiyo ni viti vya kijani ni sh. 3,000, viti vya bluu sh. 5,000, viti vya rangi ya chungwa sh. 7,000, VIP C sh.10,000, VIP B sh. 20,000 na VIP A sh. 30,000. Tiketi zitaanza kuuzwa Septemba Mosi mwaka huu.
Vituo vya kuuza tiketi ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kituo cha Mafuta cha Big Bon (Kariakoo), Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Samora na Ohio, Uwanja wa Uhuru na Kituo cha Mafuta cha OilCom Ubungo.
Mchezaji Idrisa Rajab anayechezea Sofapaka ya Kenya amewasili jana usiku na tayari ameripoti kwenye kambi ya Taifa Stars. Stars inaendelea na mazoezi Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar-es-Salaam.

MRUSI ASHINDA MASHINDANO YA 'KUPIGA KWATO'

Daegu

Katika siku ya tano mashindano ya Ubingwa wa riadha wa dunia haya kulikuwa na mashindano ya mbio za fainali za kutembea za kilomita 20 kwa wanawake. Ushindi umemwendea Mrusi Olga Kaniskina baada ya kwenda kasi ya saa moja dakika 29 na sekunde 42.
Baada ya mashindano alisema kuwa mpambano ulikuwa mkali kwake akilinganisha na mashindano ya Osaka na Berlin.Amesema kuwa kulikuwa na jua kali na hata hivyo amehimili na kushinda sasa anataka kuwa ubingwa wa Ulaya.
Nafasi ya pili ilikwenda kwa Mchina Hong LIU ambae katika mashindano ya Berlin, miaka miwili iliopita, alishika nafasi ya tatu.
Nafasi ya tatu ilikwenda Urusi .
Susana Feitur kutoka Ureno hajaishiwa nguvu licha ya kushiriki mara 11 mfululizo na bila kushinda . Amemaliza wa sita, na anaona kidogo anapiga hatua mbele kwani katika mashindano ya Berlin 2009 alikuwa wa 10.
Mkenya pekee katika mashindano haya ambayo kawaida si ya Afrika ni Grace wanjiru Njue ambae hakufua dafu karibu alikuwa wa mwisho.

ARMAND TRAORE AJIPELEKA QPR

Armand Traore

Mlinzi wa kusoto wa Arsenal Armand Traore amejiunga na vijana wapya katika Ligi Kuu ya soka ya England QPR kwa kitita ambacho hakijasemwa.
Armand Traore mwenye umri wa miaka 21, anaondoka Arsenal baada ya kuichezea klabu hiyo kwa miaka mitano akiwa ameshiriki mechi 23, amesaini mkataba wa miaka mitatu na QPR.
Traore anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na QPR chini ya mmiliki wake mpya Tony Fernandes, akifuatiwa na Joey Barton pamoja na Luke Young.
"Nilipozungumza na meneja Neil Warnock alionekana kuwa na matumaini makubwa nami katika klabu hiyo," alisema Traore.
Traore aliichezea Juventus kwa mkopo msimu uliopita, lakini akawa anatafuta nafasi ya kuwa mchezaji atakayepangwa kila mechi.
Beki huyo atavaa fulana yenye nambari 13 katika klabu hiyo ya magharibi mwa London na Warnock amesema: "Armand amekuwa mchezaji nambari moja niliyekuwa namhitaji kwa muda mrefu.

STOKE YAGONGA MWAMBA KWA LUKAKU WA CHELSEA

Romelu Lukaku

Stoke imekwama katika mipango yake ya kutaka kumsajili kwa mkopo mshambuliaji mpya wa Chelsea Romelu Lukaku kwa sababu ya kanuni za Ligi Kuu ya England.
Romelu Lukaku, aliwasili Stamford Bridge akitokea klabu ya Anderlecht mapema mwezi wa Agosti na alicheza mechi yake ya kwanza na Chelsea siku ya Jumamosi.
Lakini kanuni ya Premier League namba M 7.1 inasema: "Usajili wa muda hautawezekana wakati wa dirisha la usajili ambapo mchezaji amekuwa ndio kwanza amekamilisha usajili na klabu nyingine."
Wakati huo huo Stoke wamo mbioni kumsajili Wilson Palacios kutoka Tottenham kwa kitita cha paundi milioni 6 na kiungo huyo anajiandaa kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Stoke katika siku za karibuni pia imehusishwa kutaka kumchukua mshambuliaji wa Spurs Peter Crouch.
Na vyombo vya habari vya Denmark vimesema mshambuliaji wa Arsenal Nicklas Bendtner huenda yupo njiani kujiunga na Stoke.
Chelsea ilimsajili Lukaku kwa kitita cha paundi milioni 20 tarehe 6 mwezi wa Agosti. Ni mchezaji mashuhuri nchini Ubelgiji baada ya kuwa mfungaji bora katika ligi ya nchi hiyo msimu wa 2009-2010 alipokuwa na umri wa miaka 16.
Alifunga mabao 16 katika mechi 37 za ligi msimu uliopita na akafunga bao lake la kwanza katika mechi ya kimataifa Ubelgiji ilipoilaza Urusi mabao 2-0 mwezi wa Novemba.

Per Mertesacker kujiunga na Arsenal

Per Mertesacker

Mlinzi wa Werder Bremen anayechezea timu ya taifa ya Ujerumani Per Mertesacker anakaribia kufanyiwa uchunguzi wa afya yake katika klabu ya Arsenal.
Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 26- ambaye pia ni nahodha wa klabu hiyo ya Werder Bremen inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani maarufu Bundesliga, pamoja ya kwamba yumo katika kikosi cha timu ya taifa hivi sasa, ameruhusiwa kusafiri hadi London.
Mipango ya Arsenal kumsajili Mertesacker, mwenye urefu wa futi 6 na inchi 6 aliyekwishacheza mechi 75 kwa timu ya taifa ya Ujerumani, inaweza ikawa ndio mwisho kwa klabu hiyo kutaka kumsajili mlinzi wa Bolton Gary Cahill.
Lakini Gunners pia wamo mbioni kumsajili beki wa kushoto Mbrazil Andre Santos.
Hatua ya wa meneja wa Arsenal Arsene Wenger kuimarisha safu yake ya ulinzi, imetokana na timu hiyo kuadhiriwa kwa kuchapwa mabao 8-2 na Manchester United siku ya Jumapili katika Ligi Kuu ya England.
Hivi karibuni klabu hiyo ilimuuza mlinzi wake wa kushoto Gael Clichy kwa Manchester City, na mlinzi wa kuume Emmanuel Eboue kwa klabu ya Uturuki ya Galatasary, wakati siku ya Jumanne imemuuza Armand Traore kwa klabu ya Queens Park Rangers.
Mlinzi wa kati wa Arsenal Thomas Vermaelen aliumia akijiandaa kwa safari ya Old Trafford na msimu uliopita hakuweza karibu msimu mzima akiwa ameumia kifundo cha mguu.
Mertesacker alikuwemo katika kikosi cha Ujerumani kilichoilaza England mabao 4-1 katika Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini mwaka 2010.
Na ameitwa tena katika kikosi cha Ujerumani kitakachopambana na Austria katika mechi ya kufuzu kwa Ubingwa wa Ulaya siku ya Ijumaa baada ya kuumia kisigino mwishoni mwa msimu uliopita.

SEBASTIAN COATES AJIUNGA NA LIVERPOOL

Sebastian Coates

Liverpool imekamilisha kumsajili mlinzi wa kimataifa wa Uruguay Sebastian Coates akitokea klabu ya Nacional.
Coates mwenye umri wa miaka 20 alikuwa mchezaji nyota wa Uruguay katika mashindano ya Copa America mwezi wa Julai na amesaini mkataba wa muda mrefu katika Anfield.
Mlinzi huyo wa kati mwenye urefu wa futi 6 na inchi 6, alifaulu vipimo vya afya yake na amekwishapata kibali cha kufanyia kazi na anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Liverpool msimu huu.
Anaungana na mchezaji mwenzake wa Uruguay Luis Suarez, ambaye aliandika katika mtandao wa tweeter: "Ningependa kumkaribisha Anfield, Coates mwenzangu katika timu ya taifa ya Uruguay, rafiki na mchezaji bora," .
Meneja wa Liverpool Kenny Dalglish alikuwa na shauku ya kuimarisha ngome yake baada ya mlinzi Sotirios Kyrgiakos kujiunga na klabu ya Wolfsburg akiwa mchezaji huru.
Manchester City nayo ilihusishwa sana kutaka kumchukua Coates, lakini sasa amejiunga na kikosi cha Liverpool ambacho hivi karibuni kiliwapata wachezaji wa kiungo Jordan Henderson, Charlie Adam na Stewart Downing, mlinda mlango Doni na mlinzi Jose Enrique.

JOE COLE ATUA LILE

JOE COLE
Kiungo wa Liverpool Joe Cole amejiunga na klabu ya Lille ya Ufaransa kwa mkopo kwa msimu huu.
Cole mwenye umri wa miaka alikwenda Ufaransa siku ya Jumanne kufanyiwa vipimo vya afya yake na licha ya kutakiwa pia na klabu ya Aston Villa, amechagua kujiunga na Ligi ya Ufaransa.
Mchezaji huyo anayechezea pia timu ya taifa ya England, alijiunga na Anfield mwezi wa Julai mwaka 2010 kwa mkataba wa miaka minne akitokea Chelsea lakini ameanza kucheza mechi 11 tu kwa Liverpool.
Hakuwa kucheza mechi hata moja tangu Kenny Dalglish achukue hatamu msimu huu.



SCOTT PARKER AMWAGA WINO SPURS!

Scott Parker - Kiungo mpya wa Spurs


Tottenham imefikia makubaliano kumsajili kiungo wa timu ya taifa ya England Scott Parker kutoka klabu ya West Ham kwa kiticha cha karibu paundi milioni 5.
Hatua hiyo imekuja baada ya Parker mwenye umri wa miaka 30 kuwasilisha maombi ya uhamisho siku ya Jumanne, akieleza anataka kucheza Ligi Kuu.
Kujiunga kwa Parker na timu hiyo ya kaskazini mwa London, huenda kumemfanya Wilson Palacios ajiunge na Stoke City.
Meneja wa Spurs Harry Redknapp alisema siku ya Jumatano kwamba Luka Modric hatahama klabu hiyo.
Parker, aliyejiunga na West Ham akitokea Newcastle kwa kitita cha paundi milioni 7 mwaka 2007, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Chama cha Waandishi wa Habari za Kandanda msimu uliopita, licha ya klabu yake kumaliza mkiani katika Ligi Kuu ya England.
West Ham imesema wamekubali "kwa shingo upande" kumuachia kiungo wao huyo, licha ya jaribio lao la kutaka kumbakisha Upton Park.

TEVEZ: NITAHESHIMU MKATABA WANGU

Carlos Tevez


Carlos Tevez amekiri itakuwa "vigumu" kuondoka Manchester City kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili msimu huu.
Tevez alikuwa na matumaini angeondoka katika klabu hiyo ili aweze kuwa karibu na mabinti wake nchini Argentina.
Lakini taarifa za karibu na mchezaji huyo zimeiambia BBC: "Itakuwa haiwezekani kwa Carlos kuondoka na hilo analifahamu."
Ameongeza kusema klabu ya Inter Milan imemtaka mshambuliaji huyo, lakini imeshindwa na kiasi cha pesa walichoweka Manchester City.
Kubakia katika klabu hiyo kutaonesha kushindwa kwa mchezaji huyo ambaye mwezi wa Julai alitoa taarifa akieleza kinagaubaga nia yake ya kuachana na City kwa sababu za kifamilia.
Wiki chache baadae, City ilikuwa imeingia matumaini kwamba makubaliano na klabu ya Corinthians kumuuza mshambuliaji huyo yatakamilika, lakini baadae klabu hiyo ya Sao Paulo-ilijitoa kwa sababu haikuweza kukamilisha taratibu za uhamisho kabla kufungwa kwa dirisha la usajili wao wa kimataifa.
Inter Milan pia imekuwa ikihusishwa na mchezaji huyo, lakini badala yake wakaamua kumchukua Diego Forlan kutoka Atletico Madrid kuchukua nafasi ya Samuel Eto'o.
Mchanganyiko wa ada iliyokuwa ikitakiwa na Manchester City kwa ajili ya Tevez pamoja na mshahara wake ndio ilionekana kikwazo cha kumuuza mshambuliaji huyo.
Tevez bado hajapata nafasi ya kuanza mechi hata moja msimu huu kwa Manchester City, huku Sergio Aguero na Edin Dzeko wakionekana na Meneja Roberto Mancini wakakamavu katika safu ya ushambuliaji.
Mshambuliaji pia alipoteza unahodha wake, nafasi iliyochukuliwa na Vincent Kompany na nafasi yake katika kikosi cha timu ya Argentina imechukuliwa na Aguero.
Tevez alisaini mkataba wa miaka mitano na City mwezi wa Julai mwaka 2009, akiwa ametokea klabu ya Manchester United.
Aliwasilisha maombi ya uhamisho mwezi wa Desemba, kabla ya kuondoa maombi hayo na akaisaidia City kumaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya England.

Michael Bradley completes move to Italian club A.C. Chievo Verona

Michael Bradley
Midfielder
Fee: Undisclosed
Contract: Undisclosed
Borussia Monchengladbach midfielder Michael Bradley has completed a move to Serie A side A.C. Chievo Verona, his agent announced via Twitter on Tuesday.

"I am happy to report that Michael Bradley has signed with A.C. Chievo Verona of the Italian Serie A," agent Ron Waxman said.

Goal.com was the first to report earlier this month that a move to Italy would be in the U.S. international's future in the days leading to the transfer deadline on Aug. 31. Terms of the transfer deal were not disclosed.

Bradley's representative in Italy Paolo Alberto Faccini revealed to Goal.com that Italian teams Napoli and Roma were also interested in the player.

The move represents a fresh start for Bradley, who fell out of favor at Gladbach last year before an unsuccessful loan stint at Aston Villa. After his return to Germany this summer, it was clear Bradley was not in coach Lucien Favre's plans despite being locked down for one more year.

Bradley was also left off of Jurgen Klinsmann's latest roster for the upcoming friendlies against Costa Rica and Belguim. The new U.S. coach, who replaced Bradley's father following the Gold Cup, has said he will only call up players who consistently get minutes with their club teams.

The 24-year-old New Jersey native began his pro career at 16 in Major League Soccer with the New York/New Jersey MetroStars. He went on to play for Heerenveen in the Netherlands before making his way Gladbach.

Last season Chievo finished in 11th place on the 20-club league with an 11-14-13 record. The club begins its Serie A schedule at home on Sept. 10 against newly promoted Novara.
More On : Chievo, Mönchengladbach, Michael Bradley

 

Monday, August 29, 2011

KIPIGO CHA 'BAKORA' 8-2 CHAMSONONESHA WENGER

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger

Arsene Wenger amesema ameaibishwa kwa kuzabwa mabao 8-2 dhidi ya mahasimu wao wakubwa Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Wayne Rooney alifunga mabao matatu katika mechi hiyo ikiwa ni mara yake ya sita kupachika mabao matatu katika mechi moja kwenye uwanja wa Old Trafford huku Manchester United kwa ushindi huo wakikamata usukani wa Ligi hiyo na kumuacha Wenger akiendelea kukabiliwa na mzozo unaokuwa katika klabu ya Arsenal.
"Bila shaka unajihisi kuabishwa unapofungwa mabao manane," alisema meneja huyo wa Arsenal. "Ilikuwa siku mbaya sana."
Wenger amesisitiza ni mapema mno kusema kama sera yake ya uhamisho imeingia dosari kufuatia kuondoka kwa Cesc Fabregas na Samir Nasri na kukosa kiungo wa kuchukua nafasi zao.
Lakini hivi sasa anakabiliwa na kibarua cha kusajili wachezaji kabla ya dirisha la usajili halijafungwa siku ya Jumatano saa tano usiku.
Wenger, ambaye amesisitiza hatang'atuka, anatarajiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Monaco, ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Korea Kusini Park Chu-Young kabla muda wa usajili haujamalizika.
Pia anataka kusajili mlinzi wa kati na kiungo na Arsenal huenda ikarejea tena mbio za kumsajili mlinzi wa kati wa Bolton, Gary Cahill. Maombi yao mara ya kwanza yalitupwa.
Wenger, ambaye alianza kuwa meneja wa Arsenal mwezi wa Oktoba mwaka 1996, ameongeza kusema: "Hatuna budi kutafuta wachezaji wanaofaa na iwapo tutawapata tutawasajili. Pesa tunazo na iwapo tutawapata watakaoimarisha kikosi chetu tutafanya hivyo. Iwapo hatutafanya hivyo, basi itakuwa hatujawapata wachezaji hao wanaotufaa.
Baada ya Arsenal kufungwa vibaya mabao 8-0 mwaka 1896 ugenini na timu ya Loughborough Town katika ligi ya daraja la pili, Wenger ameongeza: "nahisi kufungwa huku kumetokana na hali maalum.
"Wachezaji wetu wengi hawachezi na tumecheza mechi tano tu. Tulichoka mwishoni lakini wachezaji wetu wanane muhimu hawakucheza."
Meneja wa Manchester United Ferguson alitoa maneno ya kufariji akisema: "Tunaishi katika dunia iliyojaa kubeuana na vyombo vya habari vya habari vipo katika mashindano ya kutojali na kuwa tayari kumalizana.
"Ni vigumu kuelewa kwa wakati huu, lakini kazi iliyofanyika miaka 15 iliyopita sasa inaonekana ni ya ajabu sana.
"Alianzisha aina ya soka ya kipekee na mtindo wa usakataji soka wa aina yake na akachukua wachezaji wanaovutia kiuchezaji na pia amefanikiwa kuuza vizuri wachezaji. Hilo naliheshimu."
Nahodha wa Arsenal Robin van Persie, ambaye alikosa kufunga mkwaju wa penalti uliookolewa na mlinda mlango wa United wakati Gunners walipokuwa nyuma kwa bao 1-0, amekiri timu yake haina budi kuimarika kabla ya mchezo ujao wa ligi utakaofanyika Emirates dhidi ya Swansea tarehe 10 mwezi wa Septemba.
"Hatuna budi kurudi katika mstari," alisema mshambuliaji huyo. "Tutakabiliana na Swansea katika wiki mbili zijazo, ambao ni wapinzani wazuri na nausubiri kwa hamu mpambano huo.
"Sidhani kama tunaweza kujificha nyuma ya kivuli cha majeruhi ama kusimamishwa wachezaji. Hakuna kisingizio. Na wao wanao majeruhi pia, hii ni soka."
Mlinzi wa zamani wa Arsenal Lee Dixon amesema Gunners tayari hawakupewa nafasi ya kutwaa ubingwa, lakini akasisitiza Wenger bado ni mtu anayefaa kwa kazi hiyo.

KIM POULSEN AITA 30 TIMU YA VIJANA

Kocha mkuu wa Timu ya Vijana, Kim Poulsen aliyevalia shati nyeusi


Kocha wa timu za vijana Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 30 wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kwa ajili ya mazoezi mwezi ujao.
 
Wachezaji walioitwa ni Saleh Ally (TSA), Jackson Wandwi (Azam), Hassan Kessy (Mtibwa Sugar), Khamis Mroki (Mtibwa Sugar), Yassin Mustapha (Polisi Dodoma), Andrew Kasembe (Moro United), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Ally Teru (Simba), Said Ruhava (Kagera Sugar), Samuel Mkomola (Azam), Frank Damayo (JKT Ruvu), Omega Seme (Yanga), Atupele Green (Yanga), Thomas Ulimwengu (ABC Sweden) na Jerome Lambele (Moro United).
 
Wengine ni Simon Msuvan (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Alex Joseph (Majimaji), Ibrahim Rajab (Azam), Renatus Patrick (Polisi Dodoma), Abdallah Kilala (AFC), Rajab Zahir (Moro United), Amani Kyata (TSA), Edward Shija (Simba), Alfred Amede (Russia), Khelf Hassan (Kenya), Emily Mgeta (TSC Mwanza), Ramadhan Salum (Simba), Frank Sekule (Simba) na Hassan Dilunga (Ruvu Shooting).

TWIGA STARS KUAGWA KESHO

Kikosi cha Twiga Stars

Timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twigs Stars) inayoondoka Agosti 31 mwaka huu kwenda Maputo, Msumbiji kwenye michezo ya All Africa Games itakayofanyika nchini humo kuanzia Septemba 3-18 mwaka huu itaagwa kesho (Agosti 30 mwaka huu).
 
Twiga Stars wataagwa saa 6 mchana kambini kwao hoteli ya Itumbi iliyopo Magomeni Mwembechai, Dar es Salaam. Wakati huo huo Kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza majina ya wachezaji 16 watakaokwenda Maputo.
 
Wachezaji hao ni Sophia Mwasikili, Fatuma Omary, Mwanaidi Tamba, Fatuma Bashiri, Mwajuma Abdallah, Asha Rashid, Mwanahamisi Omari, Pulkeria Charaji, Ester Chabruma, Zena Khamis, Fridian John, Fatuma Mustafa, Ettoe Mlenzi, Ftuma Khatib, Maimuna Said na Mwapewa Mtumwa.
 
Viongozi watakaofuatana na timu hiyo ni Mkwasa, kocha msaidizi Nasra Mohamed, daktari wa timu Dk. Gania Seif wakati Meneja wa timu hiyo ni Furaha Francis.
 
Mechi ya kwanza ya Twiga Stars itakuwa Septembe 5 mwaka huu dhidi ya Ghana wakati ya pili dhidi ya Afrika Kusini itachezwa Septemba 8 mwaka huu. Twiga Stars itacheza mechi yake ya mwisho katika hatua ya makundi Septemba 11 mwaka huu dhidi ya Zimbabwe.

TFF YATANGAZA VIINGILIO VYA STARS vs ALGERIA

Viingilio kwa ajili ya mechi ya mchujo kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon kati ya Taifa Stars na Algeria vitakuwa kama ifuatavyo;
 
Viti vya kijani ni sh. 3,000, viti vya bluu sh. 5,000, viti vya rangi ya chungwa sh. 7,000, VIP C sh.10,000, VIP B sh. 20,000 na VIP A sh. 30,000. Tiketi zitaanza kuuzwa Septemba Mosi mwaka huu.
Kikosi cha Taifa Stars
Taifa Stars tayari iko kambini tangu jana (Agosti 28 mwaka huu) na inaendelea na mazoezi Uwanja wa Karume ambapo wachezaji wote wa ndani waliripoti jana mchana na kuanza mazoezi jioni.
 
Wachezaji wan je waliofika jana usiku ni Abdi Kassim na Dan Mrwanda kutoka Vietnam na Mbwana Samata kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Athuman Machupa (Sweden), Henry Joseph (Norway) na Idrisa Rajab (Kenya) wanaingia leo jioni.
 
Nizar Khalfan wa Vancouver Whitecaps ya Canada ndiye atakayekuwa mchezaji wa mwisho kuripoti kambini. Khalfan atatua nchini kesho saa 5.15 usiku kwa ndege ya PrescisionAir akitokea Nairobi.
 

USAIN BOLT AONDOLEWA KATIKA FAINALI ZA MITA 100!

Usain Bolt akifunika uso akiwa haamini kilichotokea



Bingwa wa dunia Usain Bolt ameondolewa katika fainaili za mita 100 mashindano ya dunia mjini Daegu baada ya kuanza mbio mapema, huku raia mwenzake wa Jamaica Yohan Blake akinyakua medali ya dhahabu.
Mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt aliondolewa katika fainali za mita 100 kwa wanaume katika mashindano ya dunia ya riadha ya Daegu, Korea ya Kusini, huku raia mwenzake wa Jamaica, Yohan Blake, akipata dhahabu.
Bingwa mtetezi Bolt aliwashangaza mashabiki wengi wa riadha katika uwanja wa Daegu, alipoondolewa kwa kuanza mbio hata kabla kusikia mlio wa bunduki.
Blake aliweza kukamilisha mbio hizo kwa sekunde 9.92, akimtangulia Mmarekani Walter Dix (10.08) na bingwa wa dunia mwaka 2003, Kim Collins (10.09).
Lakini gumzo hasa ambalo linaendelea ni kumhusu Bolt, ambaye bado alitazamiwa kushiriki katika mbio za mita 200m na 4x100.
Kabla ya mbio, kama kawaida, Bolt alionekana kutulia.
Wengi watajiuliza ikiwa yaliyompata Bolt ni kufuatia sheria mpya kuanzishwa, inayohusu kuanza mbio mapema kabla mlio wa bunduki.
Kanuni hiyo ya riadha, nambari 162.7, inaelezea kwamba ikiwa mwanariadha ataanza mbio mapema kabla ya mlio huo, basi ataondolewa katika mashindano.
Kitambo, mwanariadha alisamehewa alipofanya kosa hilo mara ya kwanza, na aliondolewa katika mashindano iwapo alirudia kosa hilo mara ya pili.
Sheria hiyo mpya ilitangazwa na shirikisho la kimataifa la riadha, IAAF, mwanzoni mwa msimu wa riadha mwaka 2010.
Ijapokuwa Blake, mwenye umri wa miaka 21 alimsikitikia mwenzake Bolt, na ambaye hufanya mazoezi naye, alisema alifurahishwa sana na ushindi huo wa ghafula.
"Sidhani nina maneno ya kuelezea hayo, na ninahisi kulia machozi," alisema. "Nimekuwa nikisali kupata ushindi, na hii kwangu ni ndoto.
"Usain Bolt amekuwa akinisaida. Nilihisi nitapata ushindi kwa niaba ya Bolt."
Collins, mwenye umri wa miaka 35, na alielezea wasiwasi wake kuhusiana na sheria hiyo mpya, baada ya kupata medali yake ya shaba.
"Sidhani sheria hii ni sawa. Mambo haya hutokea na ni lazima uwape watu nafasi," alielezea mwanariadha huyo kutoka St Kitts na Nevis.
Bolt, mwenye umri wa miaka 25, amekuwa akiwika katika mbio fupi miaka michache iliyopita, tangu alipovuma na kuandikisha rekodi katika mbio za mita 100 na 200 katika mashindano ya Olimpiki 2008 na vile vile Roma, akiandikisha muda wa sekunde 9.58 na 19.19.
Baadhi ya wanariadha wazoefu wa mbio za mita 100 walikuwa wamekosekana katika fainali hizo za Daegu, ikiwa ni pamoja na wanariadha Asafa Powell, Steve Mullings, Tyson Gay na Muingereza Dwain Chambers ambaye aliondolewa katika nusu fainali, pia baada ya kuanza mbio kabla ya mlio wa bunduki.

MO FARAH ASHINDWA KUPATA DHAHABU MITA 10,000

MO FARAH

Mo Farah wa Uingereza ameshindwa kunyakua medali ya dhahabu katika mbio za mita 10,000 za Ubingwa Dunia baada ya kupitwa sekunde za mwisho kabla ya mfundo na Muethiopia Ibrahim Jeilan.
Farah, ambaye ni binadamu mwenye kasi zaidi duniani mwaka huu katika mbio hizo za mita 10,000 zenye mizunguko 25, alikuwa amelenga kuwa Muingereza wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika mbio hizo ndefu.
Katika mbio hizo alionekana kujiamini sana akiongoza mbio hizo hadi iliposalia chini ya mizunguko miwili.
Lakini ameiambia BBC: "Inauma. Kila mara unahitaji kushinda dhahabu. Hatimaye nimeambulia patupu."
Farah alikuwa akiongoza mbio hizo sehemu kubwa na alionekana hana wasiwasi huku akiongeza kasi zikiwa zimesalia mita kama 600.
Lakini Jeilan polepole alianza kupumua mgongoni mwa Farah walipokuwa wakiingia hatua ya mwisho na akampita Farah huku wakiukodolea macho mstari wa kumalizia.
Mwenzake Jeilan kutoka Ethiopia Imane Merga alishika nafasi ya tatu na kunyakua medali ya shaba, lakini Kenenisa Bekele, mshindi wa mbio za mita 10,000 kwa miaka minne iliyopita hakumaliza mbio hizo ikiwa imesalia mizunguko 10 kutokana na kuumia.
Bingwa huyo mara tatu wa Olympic Bekele, hajashiriki mbio zozote tangu mwezi wa Januari mwaka 2010 kutokana na kuumia na hakuonekana kama angetoa changamoto ya kuwania medali.