Saturday, September 3, 2011

VAN DER VAART NJE WIKI SITA!

Rafael van der Vaart - Kiungo wa Spurs.

Kiungo wa Spurs Rafael van der Vaart huenda asicheza soka kwa muda wa hadi wiki sita baada ya kuumia msuli wa paja.
Mchezaji huyo anayechezea pia timu ya taifa ya Uholanzi, aliumia wakati Tottenham ilipocharazwa nyumbani kwao mabao 5-1 na Manchester City.
Tottenham wapo mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu ya soka ya England baada ya kupoteza mechi zao zote mbili za ufunguzi dhidi ya Manchester United na Manchester City.
Meneja wa Spurs Harry Redknapp ameliambia gazeti la Sun: "Hilo ni jambo la mwisho kabisa kulisikia. Ni jeraha baya na alikuwa katika hali nzuri kimchezo."
Kiungo mshambuliaji huyo amekuwa mchezaji muhimu tangu alipojiunga na Spurs akitokea Real Madrid kwa kitita cha paundi milioni 8 mwaka 2010.
Van der Vaart atakosa mechi za Ligi Kuu dhidi ya Wolves, Liverpool na Wigan, na pia mechi dhidi ya watani wao wa jadi Arsenal katika uwanja wa White Hart Lane.
Pia hataweza kuanza kuichezea Spurs katika kampeni za ligi ya kuwania kombe la Europa, ikiwemo mechi dhidi ya PAOK Salonika na Shamrock Rovers.

No comments:

Post a Comment