Mchezaji mpya wa Arsenal Park Chu-Young.
Mchezaji mpya wa Arsenal Park Chu-Young, mchana wa leo ameiwezesha Nchi yake Korea Kusini kupata ushindi a magoli 6-0 dhidi ya Lebano.
Katika mchezo Park Chu-Young aliweza kufunga magoli matatu (hat-trick), huku magoli mengine yakifungwa na mshambuliaji mpya wa timu ya Sunderland Ji Dong-Won, huku mengine mawili yakifungwa na kiungo wa Timu ya Sangju Sangmu Kim Jung-Woo.
Kwa ushindi huo Korea Kusini, imejiweka kwenye mwanzo mzuri wa kampeni yake, kuweza kupata tiketi ya kushiriki kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
No comments:
Post a Comment