Kolo Toure.
Klabu ya Manchester City, imetaja kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki kwenye mashindano ya Kombe la Mabingwa Barani Ulaya, huku kiungo aliyesajiliwa hivi karibuni Owen Hargreaves akienguliwa kwenye kikosi hicho.
Kiungo huyo ameshindwa kujumuishwa kwenye kwenye kikosi cha wachezaji 23 wa Roberto Mancini licha ya hivi karibuni kusajiliwa na timu hiyo.
Beki Kolo Toure amejumuishwa kwenye kikosi baada ya kuwa nje ya Uwanja kwa Miezi sita kutokana na kesi iliyokuwa inamkabili ya kutumia madawa.
Mchezaji mwingine wa timu hiyo Wayne Bridge, ametoswa kwenye kikosi japo haikuelezwa sababu ya kuachwa kwake.
Kikosi Kamili cha Man City Ligi ya Mabingwa :
Makipa: Joe Hart, Costel Pantilimon, Stuart Taylor.
Mabeki: Gael Clichy, Joleon Lescott, Nedum Onuoha, Micah Richards, Aleksandar Kolarov, Vincent Kompany, Kolo Toure, Pablo Zabaleta, Stefan Savic.
Viungo: Gareth Barry, Adam Johnson, James Milner, Nigel De Jong, Samir Nasri, David Silva, Yaya Toure.
Washambuliaji: Sergio Aguero, Edin Dzeko, Carlos Tevez, Mario Balotelli.
No comments:
Post a Comment