Saturday, September 3, 2011

IJUE LINE-UP YA STARS v ALGERIA LEO!

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)

Juma Kaseja (1)
Shadrack Nsajigwa (14)
Amir Maftah (3)
Juma Nyoso (4)
Aggrey Morris (6)
Shabani Nditi (19)
Nizar Khalfan (16)
Henry Joseph (17)
Mbwana Samata (10)
Abdi Kassim (13)
Dan Mrwanda (7)
Substitutes:
Shabani Dihile (18)
Idrisa Rajab (15)
Victor Costa (20)
Nurdin Bakari (5)
Mrisho Ngassa (8)
Mohamed Rajab (11)
John Bocco (9)
Technical Bench:
Jan Poulsen- Head Coach
Sylvester Marsh- Ass. Coach
Juma Pondamali- Goalkeepers Coach
Dr. Mwanandi Mwankemwa- Team Physician
Alfred Chimela- Kit Manager
Leoplod Tasso- Team Manager
POULSEN ATAKA SAPOTI YA WATANZANIA
Kocha Mkuu wa Taifa Stars - Jan Poulsen.
TIMU ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, leo inatarajia kujimwaga dimbani kuikabili Algeria, kwenye mechi ya kufa na kupona ya Kundi D la kuwania tiketi ya kufuzu fainali za mwakani za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2012). Kwani mechi hiyo inatarajiwa kuwika leo, mishale ya saa 10:00 jioni, kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar-es-Salaam.
Stars pamoja na Algeria iliyotua nchini juzi usiku, zina pointi nne na ili kufufua matumaini ya kushiriki AFCON 2012 zitakazoandaliwa kwa pamoja na nchi za Equatorial Guinea na Gabon, ni lazima zisake ushindi wa namna yoyote ile.
Naye Nahodha wa Stars, Shadrack Nsajigwa ‘Fuso’, alisema kwamba wamejiandaa vyema na wanachoomba ni dua za Watanzania,  ili  kukamilisha malengo yao ya kuibuka na ushindi wa hapa nyumbani.
Alizidi kusema kwamba mechi hiyo itakuwa ngumu kwa sababu wapinzani wao wamejipanga kupigana kufa na kupona, kwani hutokana na kuimarisha kikosi chao pamoja na benchi la ufundi ikiwemo kuajiri kocha mpya Vahid Halilhodzic baada ya kumtimua wa awali, Rabah Saadane.
Alisema wanafahamu kwamba wanakabiliwa na mtihani, kwani wanazidi kumuomba Mungu ili waweze kushinda na kurejesha matumaini ya kufuzu fainali za Afrika.
Siku ya leo kila mchezaji amejipanga kucheza kwa juhudi na kwa kutumia faida ya uwanja wa nyumbani, na mashabiki wameombwa kumiminika kwa wingi kuwahamasisha zaidi.
Makocha wa Timu hizo mbili zitakazoshuka dimbani leo, Jan Poulsen wa Stars na Halilhozic wa Algeria walishindwa kutokea kwenye mkutano wa waandishi wa habari kama ilivyopangwa awali.
Mbali na Makocha hao kutotokea kwenye mkutano huo, kila mmoja alieleza kwamba alibanwa na  programu za kiufundi na kwamba watakuwa tayari kuzungumza baada ya kumalizika kwa mechi yao ya leo.
"Makocha wamesema kwamba wamebanwa na programu zao na hii inaonyesha ni jinsi gani mechi ya leo ni muhimu, wamesema watakuwa tayari kuzungumza baada ya mechi hiyo kuisha," alisema Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Mkutano huo kati ya makocha na wanahabari ulipangwa kufanyika saa 6:00 mchana lakini utakangazwa kuahirishwa hadi saa 8:00 mchana, na muda mfupi baadaye, Wambura akaeleza kwamba makocha hao hawataweza tena kuzungumza na vyombo vya habari.
Ili kuhakikisha ushindi unapatikana Poulsen amewaita nyota wote saba wanaocheza nje ya nchi ambao ni Athumani Machuppa, Mbwana Samatta, Nizar Khalfan, Henry Joseph, Danny Mrwanda, Abdi Kassim 'Babi' na Idrissa Rajab wakati Halilhodic amewaita wachezaji wa nje 20 na wa ndani wanne.
Mechi nyingine za Kundi D zinazotarajiwa kuchezwa leo ni Jamhuri ya Afrika ya Kati dhidi ya Morocco. Katika mechi nyingine za awali za kuwania kufuzu AFCON 2012, majirani Rwanda watawakaribisha Ivory Coast, Kenya watawavaa Guinea Bissau jijini Nairobi, Burundi watacheza nyumbani jijini Bujumbura dhidi ya Benin huku Uganda inayohitaji sare ili kufuzu watacheza ugenini dhidi ya Angola.

No comments:

Post a Comment