Thursday, September 8, 2011

TWIGA STARS, BANYANA BANYANA 2-2

Wachezaji wa Twiga Stars

Timu ya Taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) imetoka sare ya mabao 2-2 na Afrika Kusini (Banyana Banyana) katika mechi ya michezo ya All Africa Games (AAG) iliyochezwa leo Uwanja wa Machava jijini Maputo, Msumbiji.
 
Banyana Banyana ndiyo iliyoanza kupata bao kabla ya Twiga Stars kusawazisha dakika ya 25 kupitia kwa Mwanahamisi Shuruwa. Banyana Banyana ilianza kipindi cha pili kwa nguvu na kupata bao la pili. Zena Khamis aliisawazishia Twiga Stars dakika 60.
 
Twiga Stars itacheza mechi yake ya mwisho hatua ya makundi Septemba 11 mwaka huu dhidi ya Zimbabwe kwenye uwanja huo huo. Katika mechi yake ya kwanza Zimbabwe ilifungwa na Banyana Banyana mabao 4-2.

No comments:

Post a Comment