Steven Gerrard.
Mchezaji wa timu ya Liverpool Steven Gerrard, yuko karibu kurudi uwanjani baada ya kuwa nje ya dimba kwa kipindi cha miezi mitano kutokana na majeraha yaliyokuwa yanamkabili.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, ameshindwa kuichezea timu Liverpool na timu ya Taifa ya Uingereza toka mwezi wa March kutokana na upasuaji uliofanywa kwenye goti lake.
Anategemea kurudi kwenye mechi ya Ligi kuu ya Uingreza siku ambayo timu yake itakabiliana na Tottenham.
Gerrard ameueleza mtandao Liverpool "Najisikia vizuri sana, nimerudi na kwa sasa naweza hata kupiga mpira, naona mambo sasa yapo sawa. Naamini nitarudi kamili mazoezini siku ya Alhamisi ua Ijumaa."
Gerrard aliongeza: "Sitokuwepo kwenye mechi dhidi ya Stoke Jumamosi ijayo, ila naamini nitahusishwa moja kwa moja kwenye mechi yetu dhidi ya Tottenham, ila bado utabaki kuwa uwamuzi wa Kenny kama naweza kurudi uwanjani ."
"Nimekuwa na mapumziko marefu, nina nguvu na ari tena, najua nitarudi nikiwa fiti, mwenye nguvu na mwenye uchu wa hali ya juu ambao sijawahi kuwa nao". Alisema Gerrard.
No comments:
Post a Comment