Sunday, September 4, 2011

TEVEZ 'AJISAFISHA' KWA MANCINI

Carlos Tevez

CARLOS TEVEZ ameamua ‘kupiga u-turn’ na kudai uhusiano mbovu uliokuwa kati yake na kocha Roberto Mancini kwa sasa haupo na kuna upendo mkubwa kati yao. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina, alikuwa anang’ang’ania kuondoka ndani ya Manchester City kwa madai familia yake haifurahii kuishi jijini hapa.
“Ukweli ni kwamba mimi na Mancini tukawa na lugha mbovu kati yetu, kila mmoja alikuwa anasema lake. Zilikuwa lugha zisizo za ustaarabu hata kidogo.
“Unaweza kusema kama tulikuwa na upendo wa ugomvi, nami nilitaka niwe mshindi na nikawa nafanya kila jitihada ili niweze kuondokas.
“Nilikuwa nawaza mambo mabaya tu mwaka jana, lakini kwa sasa kila kitu kimemalizika kwani nina furaha mke wangu na mwanangu wapo hapa England kwa sasa,” alisema.


No comments:

Post a Comment