Sunday, September 4, 2011

SNEIJDER: NAWEZA KUJIUNGA NA MAN UTD JANUARI!

Wesley Sneijder
Kwa mujibu wa gazeti la Mirror la nchini Uingereza, Wesley Sneijder amewaeleza marafiki zake wa karibu kwamba, uwezekano wa kuhamia Old Trafford unaweza kufanyika mwezi January, licha ya mpango huo kushindikana kwenye kipindi cha usajili kilichomalizika hivi karibuni.
Gazeti hilo limeongeza kwa kuandika, uhamisho wa Sneijder ulishindikana kutokana na mahitaji ya mchezaji huyo wa kimataifa toka Uholanzi kuwa juu sana.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Uingereza mwanzoni walikubali kutoa ada ya uhamisho ya £30m kwa Inter Milan, ila gharama ziliongezeke.
Pamoja na mambo mengine, Sneijder aliwataka United kumkodishia ndege binafsi, na pia kuinunua nyumba yake ya Italy.
Gazeti hili limeeleza kwamba, hapo ndipo Bosi wa United Sir Alex Ferguson alihitaji muda zaidi kufanikisha mahitaji ya kiungo huyo mwanye umri wa miaka 27.
Ila Sneidjer amewaeleza watu wa karibu kwamba uhamishi wake kwenda  Old Trafford unaweza kufufuka mwezi January. Chanzo kimoja kilisema “Wesley alikuwa na nia ya kujiunga United, na makubalianao yalikuwa yanaenda vyema mpaka hatua za mwisho. Walishindwa kuafikina kimipango, ila binafsi yake anasema mwisho wa siku ataishia kuichezea Manchester United.” 


No comments:

Post a Comment