Monday, April 9, 2012

CHELSEA HAINA JIPYA ENGLAND

Usiku huu Chelsea imelazimishwa sare ya 1-1 na Fulham, ikitangulia kufunga kwa penalti kupitia kwa Frank Lampard dakika ya 45, lakini Dempsey akasawazisha dakika ya tano ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za mechi hiyo. Chelsea imeshuka hadi nafasi ya sita kwa pointi zake 57 baada ya kucheza mechi 33, wakati Fulham sasa ni ya tisa kwa pointi zake 43, baada ya kucheza mechi 33. Pichani ni bao la kusawazisha la Fulham likitinga nyavuni.

RATIBA YA SHUGHULI ZA MAZISHI KWA HAYATI STEVEN KANUMBA

RATIBA
Mwili wa marehemu Steven Kanumba utachukuliwa kwa msafara kutoka Hospitali ya Taifa, Muhimbili saa 2:30 asubuhi. Utapitishwa Barabara ya Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi hadi Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni ambako Misa ya kumuombea itasomwa pamoja na salamu mbalimbali kabla ya watu wote kumuaga.
Wito unatolewa kwa watu kujitokeza kwa wingi kuanzia saa 2:00 asubuhi, wakijipanga kando ya Barabara za Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi ili wautolee heshima mwili wa Kanumba wakati ukitolewa Muhimbili kwenda Leaders Club.

Saa 3:30 asubuhi, mwili wa Kanumba utapokelewa Viwanja vya Leaders, ukitanguliwa na mapokezi ya wazazi wake, viongozi mbalimbali wa serikali ambao juu yao kabisa atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal.
Saa 4:00, itakuwa ni muda wa kusoma Misa ambayo itachukua dakika 60, saa 5:00 kitakuwa kipindi cha salamu kutoka kwa watu mbalimbali.

Saa 6:00 mchana, ratiba ya kumuaga Kanumba itaanza mpaka saa 9:00 alasiri na baada ya hapo, utakuwa wakati wa kuusafirisha mwili kwa msafara kutoka Leaders Club mpaka Makaburi ya Kinondoni, msafara ukipita Barabara ya Tunisia, utakatisha Barabara ya Kinondoni kuelekea makaburini.

Saa 10:00 alasiri, mazishi yatafanyika kwa kufuata utaratibu wa imani ya marehemu.
Kamati ya Mazishi inatoa wito kwa watu watakaohudhuria shughuli ya kumzika ndugu yetu Kanumba, kuja na maua ili kumuaga kwa heshima.
Utulivu, unyenyekevu na ustahimilivu ni mambo muhimu yanayohitajika katika kipindi chote cha kumuaga mpendwa wetu Kanumba.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Sisi wote tulimpenda kwa dhati na tulitamani aendelee kuwa nasi siku zote ila Mungu aliyemleta kwa mapenzi yake ameamua kumchukua. Jina lake lihimidiwe.

                                            K.N.Y GABRIEL MTITU
                                   MWENYEKITI WA KAMATI YA MAZISHI

Wednesday, January 4, 2012

MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI: SIMBA KAMA YANGA, YADUNGULIWA MISUMARI MIWILI KWA MMOJA NA JAMHURI YA PEMBA.


 Mashabiki wa soka wakifuatilia kwa umakini wa hali ya juu mchezo kati ya Simba na Jamhuri, katika michuano ya kombe la Mapinduzi, katika uwanja wa Amaan, Jamhuri walishinda magoli 2-1.
 Wachezaji wa Jamhuri wakishangiria goli lao la kwanza dhidi ya Simba, katika pambano lililopigwa katika uwanja wa Amaan usiku wa kuamkia leo, katika mfululizo wa michuano ya kombe la Mapinduzi yanayoendelea kisiwani Unguja (Picha zote na Ali Mohammed)
 Ubao wa matokeo ukisomeka SIMBA 0, JAMHURI 1, hapa ilikuwa ni dakika ya 11.

 Benchi la ufundi la timu ya Jamhuri wakifuatilia kinachoendelea kiwanjani.
Benchi la ufundi la Simba pamoja na wachezaji wa akiba wakiwa hawaamini kinachotokea uwanjani baada ya kushuhudia timu yao ikilazwa mabao 2-1 na Jamhuri, katika pambano lililosukumizwa katika uwanja wa Amaan usiku wa kuamkia leo.
Bingwa mtetezi wa Mapinduzi Cup Simba SC imefuata njia ya yanga katika michuano ya kombe la mapinduzi baada ya jana usiku kupokea kichapo cha goli 2-1 toka kwa Jamhuri ya visiwani Zanzibar.
Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Amani Zanzibar ulishuhudia timu zote zikienda mapumziko bila ya kutingisa nyavu, na kipindi cha pili ndipo mabao matatu yalishuhudiwa, huku mawili ya kitinga katika nyavu za wekundu wa Msimbazi Simba na moja likitinga katika nyavu za Jamhuri.
Katika mchezo wa awali ulishuhudi Miembeni ikitoka na ushindi wa goli moja bila dhidi ya KMKM, na hivyo kundi A likiwa linaongozwa na Jamhuri, ikifuatiwa na Miembeni na Simba ikiwa ya tatu.
Leo ni zamu ya yanga kuzinduka pale watakapo wakabili Kikwajuni na Azam FC kucheza dhidi ya Mafunzo katika michezo ya kundi B.

Monday, October 24, 2011

MAN UTD YATANDIKWA NYUMBANI KWAKE MISUMARI 6-1, ARSENAL YAENDELEA KUJIFARIJI, CHELSEA 'PUNGUFU' YACHAPWA!

 Mario Ballotelli akishangilia goli lake la kwanza dhidi ya Man Utd.
 Mario Balotelli.
 Jonny Evans wa Man Utd akionyweshwa kadi nyekundu ilikuwa ni dakika ya 47 ya mchezo.
 Sergio Aguero akishangilia goli alilofunga.
 Mashabiki wa Man City 'wakiselebuka' na ushindi wa jana.
'Score boad' ikionyesha matokeo ya mwisho kati ya Man Utd na Man City hapo jana pambano lililopigwa ndani ya viunga vya 'OLD TRAFORD' 

Kinyume na matarajio ya Wengi, Man United walishindwa kabisa kuhimili vishindo vya majirani zao na mahasimu wao wa jadi. Hadi mapumziko City walikuwa wakiongoza kwa goli moja lililofungwa na Mario Balotelli.


Man United walicheza karibu kipindi chote cha pili wakiwa na mchezaji mmoja pungufu baada ya beki Jonny Evans kupewa kadi nyekundu kwa kumzuia Balotelli kwenda kumuona kipa wa United David De Gea.

Baada ya kutolewa kwa Evans, karamu ya magoli ilianza kwa City. Balotelli aliongeza bao la pili katika dakika ya 60. Sergio Aguero akafunga bao la tatu katika dakika ya 69. Edin Dzeko baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba alifunga bao la nne katika dakika ya 90, David Silva bao la tano na Dzeko tena kupiga msumari wa mwisho katika filimbi ya mwisho ya mchezo.

Bao pekee la kufutia machozi la United lilifungwa na Darren Fletcher katika dakika ya 81.

Matokeo haya yanaipa City pointi tatu ambazo zinaifanya kuendelea kuongoza kwa pointi tano zaidi ya United.
Robin Van Persie

Katika michezo mingine, Arsenal iliizaba Stoke City 3-1. Gervino aliandika bao la kwanza katika dakika ya 27, ingawa bao hilo lilisawazishwa na Peter Crouch. Hata hivyo Robin Van Persie ambaye alianza bechi katikika mchezo huo aliingia na kufunga mabao mawili.
Everton nayo ikicheza ugenini ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fulham. Mabao ya Everton yakifungwa na Royston Drenthe, Luis Saha na Jack Rodwell. Bao la Fulham lilifungwa na Bryan Ruiz.

Chelsea imebanwa na QPR na kuchapwa 1-0 katika mchezo uliojaa vuta nikuvute na kadi nyingi.
Bao hilo pekee la QPR limefungwa na Heidar Helgoson katika dakika ya 10 kwa mkwaju wa penati. Penati hiyo ilitokana na Helguson kusukumwa ndani ya boksi na David Luiz.

Jose Bosingwa alioneshwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Shaun Wrght Phillips, kabla ya Didier Drogba naye kutolewa uwanjani kwa kumchezea rafu Adel Taarabt.
Chelsea wangekwenda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo iwapo wangepata ushindi katika mchezo huu, kufuatia Man United kuchabangwa magoli 6-1 na Man City mapema.
Hata hivyo ushindi huu umeipeleka QPR hadi nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi kuu ya England.
Kwingineko Tottenham wakicheza ugenini wamewalaza Blackburn Rovers 2-1. Rafael Van der Vaart akifunga mabao yote ya Spurs. Bao pekee la Rovers lilifungwa na Mauro Formica.


Faurlin alikuwa mchezaji bora wa mchezo huo.

Sunday, October 23, 2011

YANGA WAKANA KUMTIMUA TIMBE

Mabingwa wa Tanzania Bara na Afrika Mashariki na Kati Yanga wamekanusha uvumi wa kumtimua kocha wao toka Uganda Sam Timbe.
Kocha wa Yanga, Sam Timbe

Timbe akuonekana kwenye benchi katika kichapo walicho toa Yanga kwa Toto Africa, huku kocha wazamani wa yanga Kostan Papic akionekana uwanjani katika mchezo huo, na kuvumishwa yuko mbioni kurejea Yanga na huenda jana angesaini mkataba wa kuitumikia Wanajangwani hao.

Katibu mkuu wa Yanga, Selestin Mwesigwa alisema klabu yake haijawahi kuwa na mpango wakumrejesha Papic mwenye hamu ya kuifundisha Taifa Stars wala kumtimua Kocha wao Sam Timbe, na kwamba wanamtambua Timbe kama kocha wao mkuu mpaka sasa.

Mwesigwa alisema, si kweli kwamba kutokuwepo kwa Timbe kwenye benchi wakati wa mechi dhidi ya Toto, kulikuwa na maana ya kwamba ametimuliwa.

"Hakuna kweli wa taarifa hizi, Timbe bado ni kocha wetu isipokuwa tu alishindwa kutokea katika mechi hiyo kutokana na matatizo ya kiafya," alisema Mwasigwa.


Katika hatua nyingine Uongozi wa mabingwa hao wa Soka Tanzania Bara, Yanga umeiandikia barua Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuomba kiwanja ambacho wanatarajia kujenga uwanja wa kisasa hivi karibuni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa klabu hiyo, Celestine Mwesiga, alisema, wameiandikia barua wizara hiyo, kutaka kupewa kiwanja cha hekari 20 katika Manispaa ya Kinondoni au Ilala, ili waweze kutimiza ndoto yao ya kutaka kumiliki kiwanja hicho cha kisasa kama ilivyo kwa klabu mbalimbali duniani.

“Tumeishafanya mawasiliano na wenzetu wa Wizara ya Ardhi kuomba kupatiwa kiwanja hicho na wameonyesha wapo tayari kutufanikishia lengo letu, hivyo tunasubiri wakati wowote watujulishe wapi wametupata,” alisema Mwesiga.

Alisema uongozi wake umejipanga kuhakikisha unajenga uwanja huo, ili Yanga iweze kupunguza gharama mbalimbali zinazolipwa kupitia viwanja wanavyochezea sasa, ili waweze kujiimarisha kiuchumi.

Akifafanua kuhusu uwanja huo, Mwesiga alisema utakuwa na bwawa la kuogelea, uwanja wa tenisi, mpira wa mikono, sambamba na hosteli kwa ajili ya wachezaji wa klabu hiyo.

SABRI RAMADHANI 'CHINA' MCHEZAJI BORA WA MWEZI VPL

Kiungo wa timu ya Coastal Union, Sabri Ramadhan ‘China’ amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Septemba katika Ligi Kuu ya Vodacom.

China alichaguliwa kutokana na kupata pointi nyingi kwenye mechi alizocheza kwa mwezi huo. Baadhi ya mechi alizopata pointi nyingi ni dhidi ya African Lyon na JKT Ruvu Stars.

Katika mechi namba 27 dhidi ya Lyon iliyochezwa Septemba Mosi kwenye Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam na timu yake kushinda bao 1-0 alipata pointi 85 kati ya 100.

Vilevile alipata pointi 89 kwenye mechi namba 33 dhidi ya JKT Ruvu Stars iliyochezwa Septemba 5 mwaka huu Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam. Coastal Union ilipoteza mechi hiyo kwa mabao 3-0.

Kwa kuibuka mchezaji bora wa Septemba, China atazawadiwa kitita cha sh. 600,000 kutoka kwa mdhamini wa ligi hiyo, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

Mchezaji bora wa Agosti alikuwa kiungo wa Polisi Dodoma, Ibrahim Massawe ambaye kwenye mechi namba 4 ya ligi hiyo dhidi ya African Lyon iliyochezwa Agosti 20 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma alipata pointi 93 ambazo hazikufikiwa na mchezaji yeyote kwa Agosti.

SI KAZI RAHISI KAMA UNAVYOFIKIRIA!

Mgeni Ally akiwa katika kipindi cha NIPE NIKUPE