Sunday, October 23, 2011

YANGA WAKANA KUMTIMUA TIMBE

Mabingwa wa Tanzania Bara na Afrika Mashariki na Kati Yanga wamekanusha uvumi wa kumtimua kocha wao toka Uganda Sam Timbe.
Kocha wa Yanga, Sam Timbe

Timbe akuonekana kwenye benchi katika kichapo walicho toa Yanga kwa Toto Africa, huku kocha wazamani wa yanga Kostan Papic akionekana uwanjani katika mchezo huo, na kuvumishwa yuko mbioni kurejea Yanga na huenda jana angesaini mkataba wa kuitumikia Wanajangwani hao.

Katibu mkuu wa Yanga, Selestin Mwesigwa alisema klabu yake haijawahi kuwa na mpango wakumrejesha Papic mwenye hamu ya kuifundisha Taifa Stars wala kumtimua Kocha wao Sam Timbe, na kwamba wanamtambua Timbe kama kocha wao mkuu mpaka sasa.

Mwesigwa alisema, si kweli kwamba kutokuwepo kwa Timbe kwenye benchi wakati wa mechi dhidi ya Toto, kulikuwa na maana ya kwamba ametimuliwa.

"Hakuna kweli wa taarifa hizi, Timbe bado ni kocha wetu isipokuwa tu alishindwa kutokea katika mechi hiyo kutokana na matatizo ya kiafya," alisema Mwasigwa.


Katika hatua nyingine Uongozi wa mabingwa hao wa Soka Tanzania Bara, Yanga umeiandikia barua Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuomba kiwanja ambacho wanatarajia kujenga uwanja wa kisasa hivi karibuni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa klabu hiyo, Celestine Mwesiga, alisema, wameiandikia barua wizara hiyo, kutaka kupewa kiwanja cha hekari 20 katika Manispaa ya Kinondoni au Ilala, ili waweze kutimiza ndoto yao ya kutaka kumiliki kiwanja hicho cha kisasa kama ilivyo kwa klabu mbalimbali duniani.

“Tumeishafanya mawasiliano na wenzetu wa Wizara ya Ardhi kuomba kupatiwa kiwanja hicho na wameonyesha wapo tayari kutufanikishia lengo letu, hivyo tunasubiri wakati wowote watujulishe wapi wametupata,” alisema Mwesiga.

Alisema uongozi wake umejipanga kuhakikisha unajenga uwanja huo, ili Yanga iweze kupunguza gharama mbalimbali zinazolipwa kupitia viwanja wanavyochezea sasa, ili waweze kujiimarisha kiuchumi.

Akifafanua kuhusu uwanja huo, Mwesiga alisema utakuwa na bwawa la kuogelea, uwanja wa tenisi, mpira wa mikono, sambamba na hosteli kwa ajili ya wachezaji wa klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment