Sunday, July 15, 2012

MATUKIO KATIKA PICHA YA UCHAGUZI WA KLABU YA YANGA UNAOENDELEA KATIKA UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE MCHANA HUU!

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akihutubian
 Chakula time
 Abel Mcharo aliyesoma dua ya Kikristo akisalimiana na Mussa Katabaro, pembeni yake kulia ni Clement Sanga, Yussuf Manji akisalimiana na Mzee aliyesoma dua ya Kiislamu na Abdallah Bin Kleb
  Godfrey Mabaga
 Mosha na Meja Ally Mayay Tembele kushoto
 Mzee Akilimali kulia
Serikali kuu; Manji na Sanga

 Saraha Ramadhan aliyeenguliwa, akiwa na John Jambele
Vijana wanaoendesha mchakato wa kura

UCHAGUZI Mdogo wa klabu ya Yanga, unafanyika leo kuanzia saa 5:00 asubuhi katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam huku kambi ya Yussuf Mehboob Manji ikipewa nafasi kubwa ya kushinda.
 
Manji anayewania Uenyekiti dhidi ya Edgar Chibura na John Jambele, juzi alitambulisha watu watano anaotaka kuchaguliwa nao leo wakati alipokuwa akihutubia mamia ya wanachama kwenye Mkutano wa kampeni, Uwanja wa Kaunda, uliopo makao makuu ya klabu, makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani.
 
Manji aliwataja watu hao kuwa ni nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na Wajumbe wanne ni Abdallah Bin Kleb, Mussa Katabaro, Lameck Nyambaya na George Manyama.
Ikumbukwe uchaguzi huo mdogo unafuatia Wajumbe wengi wa Kamati ya Utendaji iliyochaguliwa miaka miwili iliyopita, akiwemo Mwenyekiti Wakili Lloyd Baharagu Nchunga na Makamu wake, Davis Mosha kujiuzulu na watakaochaguliwa Jumapili watadumu kwa miaka miwili, kumalizia kipindi cha uongozi cha waliojiuzulu.
 
Manji aliwaomba wanachama wa Yanga pamoja na kumchagua yeye Jumapili, pia wawachague na watu hao watano, Sanga, Katabaro, Bin Kleb, Nyambaya na Manyama, kwani ni watu ambao anaamini atafanya nao kazi vizuri na kwa ufanisi.
 
Alisema iwapo akichaguliwa watu hao na mambo yakawa mabaya klabuni, atakuwa tayari kujiuzulu lakini akasema atasikitika iwapo atachaguliwa pamoja na watu tofauti nao hao.
Alisema katika kipindi hiki ambacho klabu haina uongozi, watu hao watano wamekuwa wakimsaidia kujenga timu kama kusajili na kadhalika kwa kujitolea hivyo ana imani nao kwa kiasi kikubwa.
 
Shughuli hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa wanachama Vijana wa Yanga, Bakili Mohamed Makele na Mwenyekiti wa Wazee, Mzee Ibrahim Ally Akilimali, ambao waliwaomba wana Yanga kuchagua timu hiyo na mambo yatakuwa mazuri.
Umati wa wanachama wanaokadiriwa kufika 2000 au zaidi ulihudhuria mkutano huo na wakati wote walikuwa wakishangilia hotuba, kuonyesha kwamba wanaafiki.
PICHA KWA HISANI YA  http://bongostaz.blogspot.com/


No comments:

Post a Comment