Monday, October 24, 2011

MAN UTD YATANDIKWA NYUMBANI KWAKE MISUMARI 6-1, ARSENAL YAENDELEA KUJIFARIJI, CHELSEA 'PUNGUFU' YACHAPWA!

 Mario Ballotelli akishangilia goli lake la kwanza dhidi ya Man Utd.
 Mario Balotelli.
 Jonny Evans wa Man Utd akionyweshwa kadi nyekundu ilikuwa ni dakika ya 47 ya mchezo.
 Sergio Aguero akishangilia goli alilofunga.
 Mashabiki wa Man City 'wakiselebuka' na ushindi wa jana.
'Score boad' ikionyesha matokeo ya mwisho kati ya Man Utd na Man City hapo jana pambano lililopigwa ndani ya viunga vya 'OLD TRAFORD' 

Kinyume na matarajio ya Wengi, Man United walishindwa kabisa kuhimili vishindo vya majirani zao na mahasimu wao wa jadi. Hadi mapumziko City walikuwa wakiongoza kwa goli moja lililofungwa na Mario Balotelli.


Man United walicheza karibu kipindi chote cha pili wakiwa na mchezaji mmoja pungufu baada ya beki Jonny Evans kupewa kadi nyekundu kwa kumzuia Balotelli kwenda kumuona kipa wa United David De Gea.

Baada ya kutolewa kwa Evans, karamu ya magoli ilianza kwa City. Balotelli aliongeza bao la pili katika dakika ya 60. Sergio Aguero akafunga bao la tatu katika dakika ya 69. Edin Dzeko baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba alifunga bao la nne katika dakika ya 90, David Silva bao la tano na Dzeko tena kupiga msumari wa mwisho katika filimbi ya mwisho ya mchezo.

Bao pekee la kufutia machozi la United lilifungwa na Darren Fletcher katika dakika ya 81.

Matokeo haya yanaipa City pointi tatu ambazo zinaifanya kuendelea kuongoza kwa pointi tano zaidi ya United.
Robin Van Persie

Katika michezo mingine, Arsenal iliizaba Stoke City 3-1. Gervino aliandika bao la kwanza katika dakika ya 27, ingawa bao hilo lilisawazishwa na Peter Crouch. Hata hivyo Robin Van Persie ambaye alianza bechi katikika mchezo huo aliingia na kufunga mabao mawili.
Everton nayo ikicheza ugenini ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fulham. Mabao ya Everton yakifungwa na Royston Drenthe, Luis Saha na Jack Rodwell. Bao la Fulham lilifungwa na Bryan Ruiz.

Chelsea imebanwa na QPR na kuchapwa 1-0 katika mchezo uliojaa vuta nikuvute na kadi nyingi.
Bao hilo pekee la QPR limefungwa na Heidar Helgoson katika dakika ya 10 kwa mkwaju wa penati. Penati hiyo ilitokana na Helguson kusukumwa ndani ya boksi na David Luiz.

Jose Bosingwa alioneshwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Shaun Wrght Phillips, kabla ya Didier Drogba naye kutolewa uwanjani kwa kumchezea rafu Adel Taarabt.
Chelsea wangekwenda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo iwapo wangepata ushindi katika mchezo huu, kufuatia Man United kuchabangwa magoli 6-1 na Man City mapema.
Hata hivyo ushindi huu umeipeleka QPR hadi nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi kuu ya England.
Kwingineko Tottenham wakicheza ugenini wamewalaza Blackburn Rovers 2-1. Rafael Van der Vaart akifunga mabao yote ya Spurs. Bao pekee la Rovers lilifungwa na Mauro Formica.


Faurlin alikuwa mchezaji bora wa mchezo huo.

No comments:

Post a Comment