Sunday, October 23, 2011

SABRI RAMADHANI 'CHINA' MCHEZAJI BORA WA MWEZI VPL

Kiungo wa timu ya Coastal Union, Sabri Ramadhan ‘China’ amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Septemba katika Ligi Kuu ya Vodacom.

China alichaguliwa kutokana na kupata pointi nyingi kwenye mechi alizocheza kwa mwezi huo. Baadhi ya mechi alizopata pointi nyingi ni dhidi ya African Lyon na JKT Ruvu Stars.

Katika mechi namba 27 dhidi ya Lyon iliyochezwa Septemba Mosi kwenye Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam na timu yake kushinda bao 1-0 alipata pointi 85 kati ya 100.

Vilevile alipata pointi 89 kwenye mechi namba 33 dhidi ya JKT Ruvu Stars iliyochezwa Septemba 5 mwaka huu Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam. Coastal Union ilipoteza mechi hiyo kwa mabao 3-0.

Kwa kuibuka mchezaji bora wa Septemba, China atazawadiwa kitita cha sh. 600,000 kutoka kwa mdhamini wa ligi hiyo, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

Mchezaji bora wa Agosti alikuwa kiungo wa Polisi Dodoma, Ibrahim Massawe ambaye kwenye mechi namba 4 ya ligi hiyo dhidi ya African Lyon iliyochezwa Agosti 20 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma alipata pointi 93 ambazo hazikufikiwa na mchezaji yeyote kwa Agosti.

No comments:

Post a Comment